Mark 7:24-30

Imani Ya Mwanamke Msirofoinike

(Mathayo 15:21-28)

24 aNdipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha. 25 bMara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake. 26Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria.
Kulikuwa na Foinike ya Siria (ndio Shamu) na Foinike ya Libya.
Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.

27Yesu akamwambia, “Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

28Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.”

29Ndipo Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, nenda zako nyumbani; yule pepo mchafu amemtoka binti yako.”

30Akaenda zake nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, yule pepo mchafu akiwa amemtoka.

Copyright information for SwhNEN